Agosti 7, 2018 Baada ya kiu ya muda mrefu, sasa wateja wa DStv wataanza tena kushuhudia moja ya ligi maarufu kabisa duniani – Ligi ya Italia – Serie A sasa MultiChoice imetangaza habari njema kuwa kuanzia msimu huu, ligi hiyo itaonyeshwa mubashara kupitia DStv.
Mbali na Serie A ambapo atakuwepo nguli wa soka Cristiano Ronaldo, wateja wa DStv wataendelea kufurahia ligi na michuano mikubwa mingi duniani ikiwemo Ligi ya Uingereza (Premier League) na La Liga.
Mbali na habari za kurudi kwa Serie A, DStv
pia itaongeza maudhui zaidi katika soka msimu huu. Watumiaji wa DStv
Bomba, wataweza kuona zaidi ya mechi 100 katika michuano ya Serie A na
Ligi Kuu ya Uingereza, huku wateja wa DStv Family wao watakuwa wakipata
mechi zote 380 za michuano ya Serie A na mechi zaidi ya 120 kutoka Ligi
Kuu ya Uingereza.
Watumiaji wa kifurushi cha DStv Compact, Compact Plus na wateja wa Premium watakuwa na upatikanaji wa mechi zote za Premium League, Serie A na mechi zote 380 za La Liga.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa soka,, Meneja uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo
alisema wateja wa DStv watapata fursa ya kufurahia msimu huu mpya wa
soka na katika kunogesha zaidi amesema michuano ya ligi ya uingereza
itatangazwa kwa lugha ya kiswahili.
Amesema pia huduma ya DStv Now
ambayo inamuwezesha mteja kutazama DStv popote alipo itawafanya
watanzania wengi kufurahia msimu huu wa soka kwani unachotakiwa tu ni
kuwa na akaunti yako ya DStv na unaweza kutazama katika vifaa zaidi ya
vinne kama vile simu, kompyuta, na televisheni ya kawaida.
Watangazaji
maarufu wa Soka hapa nchini (kutoka kushoto) Maulid Kitenge, Aboubakar
Liongo, Edo Kumwembe na Ephraem Kibonde wakiwa katika uzinduzi wa msimu
mpya wa soka watangazaji hao watakuwa wakiwaletea matangazo ya ligi kuu
ya uingereza msimu huu kwa kiswahili.
0 comments:
Post a Comment