Thibaut hajaripoti mazoezini toka fainali za Kombe la Dunia 2018 zimalizike na siku yake ya mapumziko ilikuwa inaisha juzi hivyo jana August 6 alitakiwa kuwa mazoezini na wenzake kama kawaida, leo ameripotiwa pia kutofika mazoezini kwa mara ya pili mfululizo bila sababu za msingi wakati Chelsea hawataki kumuachia chini ya pound milioni 45.
Iliripotiwa kuwa staa huyo amegoma ili kuishinikiza club yake ya Chelsea imuuze kwenda Real Madrid ambao wanamuhitaji kwa dhati, kamati ya nidhamu ya Chelsea inatajwa kukaa na inawezekana staa huyo akapigwa faini na club yake ya pound 200000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 590.
0 comments:
Post a Comment