Yanga
itashuka dimbani Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Agosti 19 2018 kumenyana na Alger
kutoka Alger wakiwa na kumbukumbu mbaya katika mechi ya mkondo wa
kwanza.
Yanga
iliruhusu mabao manne kwa sufuri huko Algiers, Algeria na mpaka sasa ikiwa ina
alama moja pekee katika kundi ambalo timu zingine zilizopo ni Rayon Sports ya
Rwanda na Gor Mahia FC ya Kenya.
Kuelekea mechi
hiyo, Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera, anaamini Yanga wanaweza wakafanya vizuri
dhidi ya wapinzani wao.
Zahera ana imani
hiyo kulingana na mazoezi anayowapa vijana wake akizingatia kufanyia marekebisho
juu ya mapungufu kadhaa ambayo yamejitokeza katika mechi zilizopita za
mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment