Tuesday, August 14, 2018



Paris St-Germain wanaandaa pauni milioni 100 kwa ofa ya mchezaji wa Tottenham mwenye miaka 26 raia wa Denmark Christian Eriksen. (Express)

Schalke wana nia ya kumasaini mchezaji mwenye miaka 22 raia wa England Reuben Loftus-Cheek kwa mkopo lakini Chelsea haunda wasiruhusu kuondoka kwake. (Telegraph)

Beki wa Manchester United Matteo Darmian anataka kuondoka Old Trafford na Juventus, Napoli na Internazionale wanamwinda mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Italia. (Manchester Evening News)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho aliachanganyikiwa kufuatia madai ya Paul Pogba ya kuwepo uhusiano mbaya kati yao siku ya Ijumaa. (Telegraph)

Kipa Marcus Bettinelli, 26, anaweza akaamua kuondoka Fulham baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza mechi ya kwanza ya msimu. (Mail)

Liverpool watasikiliza ofa kwa mchezaji wa maiaka 32 mlinzi rauia wa Estonia Ragnar Klavan. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Sunderland mwenye miaka 30 Lee Cattermole huenda akahamia Bordeaux, ambapo aliyekuwa meneja wa zamani wa Black Cats sasa ndiye meneja. (Teamtalk)

Wale wanaolengwa kuchukua nafasi ya mkurugenzi mpya wa Manchester United ni pamoja na kipa Edwin van der Sar, mkurugenzi wa Juventus Fabio Paratici na Monchi, mkurugenzi wa zamaniawa Sevilla na sasa Roma. (Independent)

Mshambuliaji Wilfried Zaha anasema bado anazungumza na Crystal Palace kuhusu kuongezwa mkataba wake huko Selhurst Park. (Mail)

Meneja wa zamani wa Argentina Jorge Sampaoli anataka kurudi kwenye usimamizi na Mexico. (Goal)

Paris St-Germain na Monaco wanataka kiungo wa kati wa Sevilla mwenye miaka 29 Mfaransa Steven Nzonzi. (France Football)

Kutoka BBC

0 comments:

Post a Comment