Aliyekuwa
meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameoneshania ya kuhitaji
kuifundisha klabu ya Manchester United na kurithi mikoba ya Jose
Mourinho msimu ujao wa ligi.
Kwa mujibu wa gazeti la L’Equipe kutoka nchini Ufaransa Daily Mil, METRO na Mirror vimesema kuwa Zidane anajipanga kutua ligi ya Uingereza hasa ndani ya klabu ya Manchester United.
Zidane
ambaye ni raia wa Ufaransa aliiyacha klabu yake ya Madrid baada ya
kuipatia jumla ya mataji matatu mfululizo ya michuano ya klabu bingwa
barani Ulaya.
Mfaransa
huyo aliwahi pia kuhusishwa na kuhitaji kuinoa timu yake ya taifa
lakini meneja Didier Deschamps aliamua kuendelea na majukumu yake mara
baada ya kutwaa ubingwa wa dunia nchini Urusi.
Mourinho
ameingia kwenye mgogoro na makamu mwenyekiti wa Old Trafford, Ed Wood
kwenye kipindi cha maandalizi ya kuanza msimu mpya ligi kufuatia
kulalamikia kukosa kusajili wachezaji wliyowahitaji.
Historia
yake ya kutomaliza misimu mitatu ndani ya klabu moja imekuwa
nichangamoto kubwa kwa Mreno huyo, hata hivyo amefanikiwa kuibuka na
ushindi wa mabo 2 – 1 dhidi ya Leicester City kwenye mchezo wake wa
kwanza wa ufunguzi wa kombe la ligi siku ya Ijumaa.
Tayari
mshindi wa kombe la dunia mwaka 1998, Zidane akiwa na umri wa 46
amejiwekea rekodi nzuri baada ya kushinda mataji matatu mfululizo ya
klabu bingwa barani Ulaya akiwa na Real, akichukua taji la La Liga, UEFA
Super Cup mara mbili na FIFA Club World Cup mara mbili.
0 comments:
Post a Comment