Thursday, September 6, 2018


Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amefunguka kuhusu tuzo za mchezaji bora wa Dunia Ballon d’or na kusema kuwa ni za ‘ajabu’

Mshambuliaji huyo amefunguka hao wakati anaongeza na jarida la Globoesporte kuhusu tuzo mbali mbali zinazotolewa kwa wachezaji wanaofanya vizuri duniani.
Griezmann licha ya kuzisaidia timu zake kutwaa mataji lakini hayupo kwenye orodha ya wachezaji watatu wanaowani tuzo ya mchezaji bora wa FIFA pia hakuwepo kwenye tuzo za mchezaji bora wa Ulaya UEFA ambazo zilifanyika katika mji wa Monaco.

Katika tuzo hiyo aliweza kushinda mchezaji wa klabu ya Real Madrid Luca Modric kwa kuwashinda Cristiano Ronaldo kutoka Juventus na taifa la Ureno pia mshambuliaji wa Liverpool na taifa la Misri Mohamed Salah.
Katika tuzo zinazotarajiwa kutolewa na FIFA pia za mchezaji bora mchezaji huyo hayumo kwenye orodha hiyo huku FIFA wakiwarudia wachezaji wale wale ambao ni Ronaldo,Salah na Modric licha ya kuisaidia timu yake ya taifa ya Ufaransa kutwaa taji la kombe la Dunia na klabu yake ya Atletico Madrid kushinda mataji mawili ambayo ni UEFA europa League pamoja na UEFA Super Cup 2018/19.

Griezimann amesema: “Ni za ajabu kwani Tuzo ni kwa mchezaji bora duniani, ila Kwa mimi na kwa Messi kwa sasa, ni Kama ilivyo katika miaka iliyopita”

“Wakati huu tulipo hapa, inapoteza uaminifu sana Haijalishi ni nani anayeshinda Kombe la Dunia au Ligi ya Mabingwa” huku akimtolea mfano Messi kuwa “Ni mchezaji bora muda wote”

0 comments:

Post a Comment