Pambano la Mwakinyo na Eggington la uzito wa kati lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano kubwa la Amir Khan dhidi ya Samuel Vargas. Khan alishinda kwa tofauti ya alama dhidi ya Vargas.
Mwakinyo aliingia katika uga wa Arena Birmingham, jijini Birmingham Uingereza kama mbadala wa bondia mengine aliyetakiwa kupambana na Eggington kushindwa kufikia vigezo.
Wachambuzi wengi wa masuala ya masumbwi waliliona pambano hilo kuwa rahisi kwa Eggignton ambaye alikuwa na rekodi bora zaidi. Wakati Mwakinyo akiwa na rekodi shinda mapambano 11 na kupigwa mawili, mpinzania wake alikuwa ameshinda mapambano 24 na kupigwa manne. Eggignton pia ni bingwa wa zamani wa Uingereza, Ulaya na nchi za Jumuiya ya Madola.
ARENA BIRMINGHAM,
BIRMINGHAM
PIC;LAWRENCE LUSTIG
Super-Welterweight contest
SAM EGGINGTON v HASSAN MWAKINYO
“Yeye (Eggington) aliingia ulingoni akiwa mwenye kujiamini sana. Nilitaka kuonesha uwezo wangu, sie wengine ni mabingwa pia lakini hatuonekani kutokana na mzingira tunayoishi,” alisema Mwakinyo baada ya pambano hilo na kuongeza: “Nimefurahi sana kwa ushindi huu na nimeionesha dunia uwezo wangu halisi.”
“Sasa nataka kupambana na Kell Brook, na na nikishamchapa namtaka Amir Khan.” Alipoulizwa kama wataweza kustahmili nguvu za Brook akajibu kwa kujiamini: “Kwani wanionaje?
0 comments:
Post a Comment