Thursday, September 13, 2018


Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ameghadhibika baada ya kusikia mipango ya aliyekuwa kocha wao,  Zinedine Zidane kutaka kuinoa Manchester United.

Perez anaamini Zidane anahitaji kuifundisha Manchester United kwa udi na uvumba hali inayomfanya rais huyo kuchukizwa wakati hakutimuliwa Real Madrid.
Zidane kurudi kazini hivi punde, atangaza kutua Old Trafford na wachezaji hawa hatari
Zidane ameachana na Madrid baada ya miaka mitatu ya ufalme wake Bernabeu na kuipatia mataji matatu mfululizo ya UEFA Champions League huku Perez alitumaini angeendelea kusalia klabuni hapo.
Zinedine Zidane Manchester United
United yakanusha ujio wa Zidane ‘Kwa nini tumzungumzie wakati hakuna nafasi ya kazi’
Mfaransa huyo anatarajiwa kuchukua mikoba ya Jose Mourinho ndani ya klabu ya Manchester United ikiwa ni mara ya kwanza kurejea tena kwenye soka la ufundishaji tangu kuachana na Madrid.
Kwa mujibu wa gazeti la nchini Hispania El Confidencial, limesema kuwa maamuzi ya Zidane kurejea na kuifundisha Man United kumemkera rais wa Real Madrid, Perez.
Zinedine Zidane Manchester United
Perez amesema kuwa amechoshwa na kusikia maswala ya Zidane kwakuwa alitarajia angechukua walau mwaka mmoja kabla ya kutangaza kurejea tena kwenye soka.
Zinedine Zidane kurithi mikoba ya Mourinho Manchester United
Haya yanakuja baada ya Mfaransa huyo kuthibitisha kuhitaji kazi kwa kuwaambia watu wake wa karibu kuwa hivi karibuni atarudi.

0 comments:

Post a Comment