Huu ndiyo mpira utakao tumika UEFA Nations League, leo Ufaransa vs Ujerumani
Kuelekea michezo ya ufunguzi ya michuano mipya ya UEFA Nations League itakayopigwa leo Septemba 6 tayari mpira rasmi utakao tumika umewekwa hadharani.
Washirika wa UEFA kampuni ya Adidas ndiyo imetumika katika mpira huo ambao utatumika katika michuano hiyo inayo jumuisha jumla ya mataifa 55 ikiwemo England itakayo ivaa Hispania siku ya Jumamosi kwenye dimba la Wembley.
Lengo kubwa la UEFA kuanzishwa kwa michuano hiyo ya Nations League ni kuondokana na taratibu za michezo ya kirafiki ambayo imeonekana kutopewa uzito mkubwa na badala yake kuja na mashindano ambayo yataleta ushindani wa kweli kwa timu zinazotoka bara hilo.
Michezo ya awali inaanza leo kwa kuikutanisha miamba ya soka ambao ni mabingwa wa kombe la dunia mwaka huu timu ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani siku ya Alhamisi.
Kunako Ijumaa taifa dogo duniani, Albania itashuka dimbani kuwakabili Israel huku Italia ikiwa mwenyeji dhidi ya Poland wakati mchezo wa mwisho ukiwa ni baina ya Uturuki watakao wavaa wenyeji wa michuano ya kombe a dunia mwaka huu timu ya taifa ya Urusi.
Kunako Ijumaa taifa dogo duniani, Albania itashuka dimbani kuwakabili Israel huku Italia ikiwa mwenyeji dhidi ya Poland wakati mchezo wa mwisho ukiwa ni baina ya Uturuki watakao wavaa wenyeji wa michuano ya kombe a dunia mwaka huu timu ya taifa ya Urusi.
Kwenye michuano hiyo inayotarajiwa kuwa na mvuto mkubwa kutokana na ukubwa timu zinazo shiriki siku ya Jumamosi Uswis itakuwa na kibarua dhidi ya Iceland wakati Finland ikicheza na Hungary huku taifa pendwa katia soka England wakiwa na kibarua kigumu mbele ya Hispania.
Miamba ya soka ya Ujerumani wakishuka Jumapili kuwakabili Peru wakati Ufaransa ikicheza na Netherlands huku Bulgaria wakiiva Norway na Denmark wakicheza mbele ya Wales.
0 comments:
Post a Comment