Tuesday, September 4, 2018



Klabu ya Real Madrid  ina nia ya kumtoa Marcelo kwa timu ya Juventus  ili wampate Alex Sandro kutoka klabu hiyo mnamo usajili wa dirisha dogo mwezi Januari mwaka kesho.

Kwa mujibu wa gazeti la  Tuttosport, Marcelo hana uhusiano mzuri na kocha wa timu yake,  Julen Lopetegui, hasa baada ya kumpumzisha katika mchezo dhidi ya Girona.

Pia kuna hisia kwamba mchezaji huyo wa Brazil anataka kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani, Cristiano Ronaldo, aliyehamia klabu hiyo msimu huu.

0 comments:

Post a Comment