Tuesday, September 4, 2018


Modric, Ronaldo, Salah hawa tena kwenye tuzo za Fifa. Watu wanaguna kwanini Griezmann na Mbappe hawapo! Swali linakuja kwanini hawapo?
Nadhani mchezaji bora wa Ufaransa kombe la dunia kwangu mimi ni Varane au Mbappe. Griezmann alikuwa na msimu wenye mafanikio lakini siamini kama alikuwa na msimu bora binafsi kumshinda Salah. Kuna tofauti ya mafanikio ambayo mtu anapata kutokana na timu hake kuwa bora na kuna mafanikio yanayotokana na mchezaji mwenyewe.


Mimi sina shaka na kabisa ila nina dukuduku kwa Ronaldo.

Mimi nadhani Ronaldo hakwenda kwenye tuzo za UEFA kwa makusudi.
Kwanini hakwenda?
Hakuna sababu iliyoanishwa maana baadae tulimuona uwanjani.
Kuna mtu ataleta hoja kuwa mbona Messi hakwenda?
Kwa logiki ya kawaida Messi amesusa kwa sababu alijua hawezi kushinda na hakukuwa na swahiba wake hata mmoja ambaye labda tungesema angeenda kusheherekea nae na kumtia moyo. Miaka ya nyuma Messi alikuwa na akina Xavi na Iniesta ambao wote walijua fika wasingeweza kubeba hiyo tuzo mbele yao lakini kwa kuwa ni swahiba wao walienda tu kutimiza ratiba.


Lakini Ronaldo kabla ya sherehe ilisemekana kuwa tayari alikuwa na ratiba na kiti chake kilishaandaliwa. Inaonekana kuna mtu alimweleza kuwa kwenye tuzo sio mshindi.

Nimesikia kauli ya Ramos. Ramos anasema kuwa
“Ronaldo hana furaha. Lakini sio kwa sababu Modric ameshinda ila ni kwa sababu hajashinda tuzo ya mchezaji bora wa uefa”
Hii inaashiria ubinafsi wa kitoto kwa nyota mkubwa kama Ronaldo. Ni aibu kususa kisa unekosa moja kati ya 5.
Ramos anasema “Nadhani kama kuna mchezaji bora alistahili tuzo hii bila shaka ni Luka Modric”

Na ukitaka kujua kuna utoto nyuma yake angalia jinsi Mendez anang’aka kuwa ni dharau. Kwa hiyo Modric kushinda hiyo tuzo ni dharau?****. Ni kweli Modric sio klasi ya Ronaldo lakini tuzo sio klasi tunaangalia fomu ya mchezaji

Mo Salah alikwenda na hakuwa na kiashiria chochote kikubwa alichompiku nacho Ronaldo kimafanikio lakini amekwenda. Kwanini ameonesha ukomavu. Na Salah hakuwa na swahiba ila amekwenda tu kuonesha uanamichezo.

Ronaldo ameonesha uroho kitu ambacho kitamnyima heshima kwa tuzo inayokuja.
Ronaldo na wachezaji wengine wenye tabia hizo ndani na nje ya taifa letu kuwa anapaswa ajue kuwa ubora wa mchezaji sio kufunga pekee yake. Wapo wanaopambana na wengine wa apewa kadi nyekundu ili yeye tu afunge. Ronaldo na wengine wasijione kwamba wao ni bora zaidi.

Sio kweli kwamba Ronaldo ni zaidi ya Real Madrid hata kama alifunga magoli 50 lakini pia alikuwa ndani ya timu bora duniani. Ronaldo ajue kuwa Madrid ndiyo chanzo kikubwa cha mafanikio yake. Zidane nae pia ni chachu ya mafanikio yake.

Kuna watu watasema kuwa Ronaldo ndiye kila kitu cha Madrid. Hapana. Kama ingekuwa ni rahisi hivyo. Kwanini asifanye hivyo kuanzia msinu wa 2009 mpaka 2014? Alikaa na Mourinho miaka kadhaa na hawakubeba makombe mengi. Anapaswa aheshimu wenzake, makocha na uongozi wa Madrid kwa ujumla. Nimeona juzi amewapotezea Madrid kwa kuwa unfollow instagram.

Kwamba anaonesha chuki za wazi kisa tu wamemwachia aondoke. Ilikuwa lazima aondoke tu haijalishi muda hata yeye alipishwa ili tu maisha yasonge. Ana miaka 34 aridhike mpira ni mchezo wa kijiti. Wengi walitamani asali ya giningi.

Hata kama wamemtenda ubaya hapaswi kuwalipa ubaya maana wamemfanya afanye makubwa zaidi ya ubaya wake.

Kama alijua tuzo ijayo hatoshinda na pia najua alifahamu kuwa wachezaji wa Madrid baadhi watabeba tuzo. Angeenda kuwasapoti kama yeye alivyosapotiwa nao na kuoneshwa upendo.

Ana mafanikio sawa lakini ni mroho. Juzi nimeona Leo Messi akipata penati ya kukamilisha Hat trick lakini akampa Suarez. Haijalishi wewe shabiki wa Ronaldo utajisikiaje lakini ingekuwa imemtokea Ronaldo asingekubali kumpa benzema hiyo penati.
Tuzo sio mabao tu, hata wale wa ndani pia wana nafasi ya kutwaa tuzo hiyo endapo watatoa burudani maridhawa ambayo imeongeza nakshi kwenye mafanikio ya klabu. Hata hivyo hayo mabao asilimia 90 Ronaldo kafunga ndani ya box la penati je huo mpira umefikaje hapo kwenye box? Kuna watu walifanya kazi.

Kwa dharau aliyowaoneshea UEFA anapaswa sio soka, maana amekwishajiona ni kama ana miguu 22 na yote inacheza uwanjani.

0 comments:

Post a Comment