Mfaransa
huyo, Mbappe amewahi kufanya majaribio ‘the Blues’ akiwa na umri wa
miaka 13 na kuitumikia timu ya vijana ili kuendelea kuonyesha uwezo
zaidi.
Lakini kwa mujibu wa Boga, klabu
hiyo ya ligi kuu England haikuvutiwa na kiwango alichokionyesha na
hivyo kumuomba kurudi kwa awamu nyingine kwaajili ya majaribio lakini,
Fayza Lamari ambaye ni mama mzazi wa mchezaji huyo akakataa.
”Nilimleta
yeye na familia yake, alikuwa mwenye ujuzi kama aliyo nao hivi sasa na
alicheza dhidi ya Charlton na kushinda mabao 7 – 0,” amesema Boga.
Boga
ameongeza ”Katika ile wiki yake akiwa Chelsea, tulikwenda ofisini na
kumuambia tumekiona kipaji chake lakini tunakualika urudi tena kwa mara
nyingine ujekufanyiwa majaribio na baada ya hapo tutajua chakufanya,”.
”Nakumbuka
ile siku mama mzazi wa Mbappe alisema kwa Kifaransana nikajaribu
kutafsri kwa lugha ya Kiingereza, ambapo aliniambia, sikiliza kijana
wangu hawezi kurudi na kama mnamuhitaji mnalazimika kumchukua sasa miaka
mitano ijayo itawagharimu euro milioni 50 kumnunua.”

Boga
ambaye alilazimika kutafsri alichozungumza, Fayza amesema kuwa licha ya
kijana huyo kuonyesha kiwango cha hali ya juu, katika soka la England
kwa wakati huo lilikuwa likihitaji wachezaji wanaotumia nguvu na juhudi
kitu ambacho Mbappe alikuwa hana hivyo kumpatia muda mwingine wa kuja
kwa majaribio ili kuona namna ya kuboresha uwezo wake.
0 comments:
Post a Comment