Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 nchini Cameroon.
Katika mchezo huo mashibiki wa soka wameshuhudia kipindi cha kwanza wenyeji Uganda wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara huku ukionekana kubadilika kwenye kipindi cha pili ambapo Stars nao wakilisakama lango la timu pinzani.
Kwa matokeo hayo sasa Uganda inaongoza kundi hilo ‘L’ kwa kuwa na jumla ya pointi nne wakati Stars ikishika nafasi ya pili kwakuwa na alama mbili huku Lesotho ikiwa ya tatu kwakuwa na pointi moja na Cape Verde ikiburuza mkia.
Kwa mechi hiyo Stars imebakiwa na michezo minne ya nyumbani na hivyo italazimika kutumia nafasi hiyo ili kujihakikishia kusonga mbele kwenye hatua inayo fuata.
0 comments:
Post a Comment