Kocha wa Real Madrid, Julen Lopetegui
Lopetegui amevunja sheria hiyo wikiendi hii baada ya kukubali kikosi chake cha Madrid kupoteza mbele ya Alaves na hivyo kuyafanya maisha yake ndani ya timu hiyo kuwa rahani.
Mourinho na rais wa Madrid, Florentino Perez
Mpaka
sasa meneja huyo ameshapoteza michezo minne mfululizo pasipo kushinda
hivyo wachambuzi wa maswala ya soka wanaamini anamuda mchache mno
usiozidi hata mwezi mmoja kuendelea kuwa kwenye timu hiyo.
Gazeti maarufu la michezo nchini Hispania la ‘Diario AS‘ kwenye kurasa zake za mbele limeandika kuwa kocha huyo kama atachukua muda mrefu Real basi ni mpaka mechi ya ‘El Clasico’ mwishoni mwa mwezi wakati.
Majina ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi yake baada ya kutimuliwa ni, Jose Mourinho, Santiago Solari anaeifundisha Real Madrid B (Real Madrid Castilla) na Antonio Conte hii ikiwa ni kabla ya Christmas au mwishoni mwa msimu.
Inafahamika
kuwa rais wa klabu ya Madrid, Florentino Perez ni rafiki na shabiki
mkubwa wa Mourinho lakini nimapema mno kumuita Mreno huyo na hivyo
anasikilizia nguvu ya mashabiki.
Conte
ni moja kati ya makocha wachache waliyokuwa kwenye listi hiyo, Solari
ambaye amewahi kuwa mchezaji wa Madrid na kocha wa kikosi B anapigiwa
upatu kuifundisha timu hiyo.
Ikiwa
baadhi ya wachezaji wakijiunga na timu zao za taifa Perez na Lopetegui
wanazidi kuwa kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kufanya usajili
mkubwa ambao utaziba pengo linaloonekana kwa sasa baada ya kumuuza nyota
wake Ronaldo kwa euro milioni 100.
Wachezaji
kama Isco, Dani Carvajal na Marcelo wakiwa wanasumbuliwa na majeraha
mara kwa mara wakati Gareth Bale na Karim Benzema wakiwa wapo chini ya
kiwango nakufanya kocha Lopetegui mwenye umri wa miaka 52 kuwa kwenye
nafasi mbaya zaidi katika kazi yake.
0 comments:
Post a Comment