Real Madrid
inapania kumsajili mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane,
lakini huenda ikashindwa kumnunua mchezaji huyo wa miaka 25 ambaye
gharama ya kumsajili ni Euro milioni 200 (El Confidencial - in
Spanish)
Manchester United inakabiliwa na kibarua kigumu
kumshawishi kipa wa Uhispania David de Gea, 27, kusalia Old Trafford
baada ya kandarasi yake ya sasa kumalizika.(Telegraph)
- Hawa ndio wachezaji bora zaidi duniani?
- Panda shuka za John Terry anapostaafu katika soka
- Kiungo wa Arsenal ashindwa kwenda Azerbaijan

Maafisa wa Manchester United walikua nchini Ureno kuwafuatilia wachezaji kadhaa wa Benfica siku ya Jumapili. (Manchester Evening News)

Mshambulizi wa Genoa Krzysztof Piatek anafahamu fika kuwa Barcelona inataka kumsajili lakini kuna fununu kwamba Manchester City, Tottenham Hotspur na Liverpool pia zinafuatilia jinsi sogora huyo wa mika 23 raia wa Poland anavyosakata kabumbu. (Diario Sport, via Talksport)

West Ham nayo inajiandaa kutangaza ofa ya mlinzi wake Declan Rice,19,- ambaye anakibali cha kuchezea mataifa ya Jamhuri ya Ireland na England - kwa kandarasi iliyo imarishwa ya karibu Euro 21,000 kwa wiki. (Football London)
Manchester City, Tottenham na Southampton wamekuwa wakimfuatilia mshambuliaji wa Sunderland Josh Maja mwenye umri wa miaka 19. (Mirror)
Daktari wa Liverpool Matt Konopinski anatarajiwa kuiacha klabu hiyo na kuenda England kuchukua wadhifa mpya baadaya ya kuwa Anfield kwa muda mrefu. (Liverpool Echo)

0 comments:
Post a Comment