Basi lililobeba kikosi cha United lilichelewa kufika katika uwanja wa Old Trafford kwa mujibu wa ratiba hali iliyopelekea mchezo huo wa kundi H kusogezwa mbele kwa dakika tano.
Polisi wagoma kukisindikiza kikosi cha Man United, Mourinho aipongeza UEFA na mwamuzi kwa huruma yao
Gari hilo la wachezaji lilitoka Lowry Hotel majira ya 6pm lakini lilichukua dakika 75 hadi kufika kwenye uwanja huo ambao upo umbali wa maili tatu kutoka walipokuwa.
Kwa mujibu wa sheria za UEFA, aina hiyo ya kosa hulimwa faini ya euro 10,000 au pauni 8,879 huku meneja wa klabu husika akikosa mechi moja.
Hata hivyo mapema mchana wa leo meneja wa United, Mourinho amewatupia lawama askari polisi wa jiji la Manchester kwa kushindwa kutoa msaada wao wa kulisindikiza basi lililobeba wachezaji jambo ambalo limesababisha kuchelewa kufika uwanjani kwa wakati.
Wakati polisi wakijibu tuhuma hizo wamesema kuwa hakuna ulazima wa kila mechi kupewa ‘escort’ na hata United walishapewa taarifa mapema miezi michache iliyopita.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.