Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema licha ya timu ya Taifa, Taifa Stars kuanza vibaya kwenye mashindano ya AFCON bado si mwanzo mbaya.
Amesema hayo leo wakati wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli azindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG ya Taifa Gas Tanzania Limited katika eneo la Vijibweni Kigamboni Jijini Dar es salaam.
"Kwenye uwanja wa mpira kuna kushinda na kushindwa kwahiyo wao wakazane, wajitume zaidi na sisi tuendelee kuwaombea, mimi nina uhakika hata huo mwanzo sio mbaya sana, kufungwa tugoli tuwili tu na timu ambayo inaongoza afrika, tuendelee kuwapa moyo" amesema.
Utakumbuka katika mchezo wa kwanza kwenye michuano hiyo ya AFCON, Taifa Stars ililala kwa magoli 2-0 dhidi ya Senegal.
0 comments:
Post a Comment