Mkufunzi
wa Chelsea Maurizio Sarri amekubali kuwa mkufunzi mpya wa Juventus na
ameitaka Chelsea kumruhusu kuondoka.(Goal). Sarri alimuelezea Marina
Granovskaia kuhusu uamuzi wake katika mkutano siku ya Ijumaa na
mkurugenzi huyo wa Chelsea aliahidi kuzungumzia hatma yake na mmiliki wa
klabu hiyo Roman Abramovich. (Sky Italy – in Italian)
Chelsea inasubiri hatua rasmi kutoka kwa mabingwa hao wa Juventus , ambao watalazimika kulipa kandarasi yake ya mwaka mmoja yenye thamani ya £5m. (Guardian).
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESBeki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, ataipatia Man United uamuzi wa uwezekano wa kuhamia katika klabu hiyo ya Old Trafford katika siku chache zijazo. (Telegraph)

Ilkay Gundogan atasalia katika klabu ya Manchester City msimu ujao hata iwapo kiungo huyo wa Ujerumani ,28, atakuwa ajenti huru wakati ambapo kandarasi yake itakamilika mwisho wa msimu huu.(Mail)
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane amezuia kuondoka kwa beki wa Uhispania Sergio Ramos, 33, . (ESPN)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESRial Madrid wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Chelsea ili kujadiliana kuhusu usajili wa Eden hazard. (Mail)

Wakati huohuo , Juventus inamlenga kinda wa klabu ya Empoli kutoka Ivory Coast Hamed Traore kama mchezaji mbadala wa Pogba. (Calciomercato)
Arsenal na Leicester wanamchunguza winga kinda wa Valencia Uhispania Ferran Torres,19, ambaye ana thamani ya £25m. (Mail)

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 30, mwisho wa msimu huu (Standard)
The Gunners wamewasiliana na Leicester kuhusu uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa klabu hiyo James Maddison lakini wamedaiwa kutaka kulipwa £60m. (Mail)
Haki miliki ya pichaREUTERSKipa wa Barcelona na Uholanzi Jasper Cillessen, 30, ameikosoa klabu hiyo kwa kuweka dau la £53million huku klabu ya Man United na Benfica zikivutiwa na mchezaji huyo. (Mail)
0 comments:
Post a Comment