Na Saleh Ally, Cairo
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameendelea kusisitiza kwamba yeye hana cha kulaumiwa.
Amunike amesema mara baada ya Stars kupoteza mchezo wake wa mwisho katika michuano Afcon.
Taifa Stars ilifungwa mechi zote tatu za michuano hiyo kwa kukubali mabao nane katika mechi tatu huku ikifunga mawili.
Baada ya mechi ya mwisho baada ya Stars kulala kwa mabao 3-0 kutoka kwa Algeria, Amunike amuse a hana cha kulaumiwa.
“Nilaumiwe
kwa lipi? Mimi ni kocha na timu uliiona. Hapo ndipo tulipofikia na
nilichofanya sikuwa na zaidi ya kuongeza,” alisema.
Hata
alipoulizwa kwamba ana maanisha hakuwa na uwezo wa kuongeza chochote cha
kuiokoa au ana maanisha hakuwa na uwezo zaidi ya hapo, akajibu.
“Mimi nimemaliza, indigo tulipofikia, ahsante.”
MECHI ILIZOPOTEZA TAIFA STARS:
Vs Senegal 2-0
Vs Kenya 3-2
Vs Algeria 3-0
0 comments:
Post a Comment