Lionel
Messi mshambuliaji wa timu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina
amesem kuwa timu yao ya Taifa imeponzwa na maamuzi ya waamuzi kwenye
mchezo wa nusu fainali ya Copa America.
Argentina
ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya Brazil kwenye hatua ya nusu fainali huku
Messi ambaye ana tuzo tano za Ballon d'Or uwanja wa Belo Horizonte usiku
wa kuamkia leo akiwa hana bahati ya kushinda kombe hilo.
Kumekuwa
na mjadala mkubwa kama Messi anaweza kuitumikia timu yake kwenye
fainali za kombe la Dunia mwaka 2022 zitakazofanyika nchini Qatar
kutokana na nyota huyo kufikisha miaka 35 mwaka huo.
Messi
amesema kuwa hawakufanyiwa sawa kwenye mchezo huo kutokana na waamuzi
kuwapotezea penalti halali ambazo walizipata kwenye mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment