Mashabiki wenye
hasira wa Korea Kusini wanataka walipwe fidia baada ya Cristiano
Ronaldo kushindwa kuingia uwanjani wakati wa mchezo wa kirafiki wa
kabla ya msimu dhidi ya Juventus.
Nyota huyo wa Ureno alikuwa
amesaini mkataba wa kucheza dakika 45 wakati mechi dhdi ya timu hiyo
ya Ligi K ya nyota wote ilipotangazwa , wanasema waandalizi, lakini
alikaa kwenye benchi nje ya uwanja. Mashabiki walijawa na ghadhabu wakati aliposhindwa kuonyesha ishara yoyote ya kuingia uwanjani, hata wakaanza kushangilia kwa kupaza sauti wakilitaja jina la hasimu wake Lionel Messi.
Baadhi ya mashabiki sasa wamekwenda hadi kwenye kampuni ya sheria mjini, inayofahamika kama Myungan kuwasilisha mashtaka.
- Uingereza yalaumiwa kutumia ''ukatili'' kuiteka meli ya Iran
- 'Kwa nini tulimkamata Kabendera'
- Mfalme wa Dubai na mkewe aliyetoroka mahakamani
- Joseph Kabila apata 'mnofu' serikali ya muungano DR Congo
"Kwa kawaida katika hali kama hii mlalamikaji hulipwa gharama ya tiketi, lakini swala hili ninalichukulia kama swala la kipekee kwasababu kampuni , kupitia matangazo ya uongo, iliwalaghai mashabiki wa nyota huyo," alisema wakili kutoka kampuni ya mawakili katika mazungumzo na shirika la habari la Reuters.
"Kwa upande wa tatizo la kuathirika kiakili , ningependa kusema kwamba baadhi yao ni mashabiki sugu, mashabiki sugu kabisa. Kwa hiyo kwao ni uchungu mkubwa kwasababu wanampenda Ronaldo na wanataka kumlinda, lakini hawawezi, kutokana na hali halisi ," aliongeza.
"Kwa sasa tuna walalamikaji ambao waliishtaki kampuni , lakini nimekuwa nikipokea simu nyingi leo na ninadhani ni zaidi ya simu 60,000 ."
Robin Chang, Mkurugenzi mkuuu wa The Fasta, wakala wa Korea walioandaa mechi hiyo aliangua kilio mbele ya waandishi wa habari wa kampuni ya SBS na kuthibitisha kuwa mkataba ulieleza wazi kuwa Ronaldo angecheza kwa dakika 45.
Hata hivyo, Bi Chang alibaini tu kwamba mchezaji huyo wa miaka 34 hatacheza mechi dakika 10 tu baada ya kipindi cha pili.
"Nilipoenda kujaribu kuzungumza na (Pavel) Nedved, naibu rais wa Juventus, kile alichoniambia ni kwamba 'pia mimi ningetamani Ronaldo acheze , lakini hataki kufanya hivyo . Samahani , hakuna ninaloweza kulifanya .' Nilisikitika sana ," alisema.
Shirika la soka la Korea Kusini Korea , K League, limesema kuwa barua ya kupinga tayari imetumwa kwa Ligi ya Championi ya Italia kwa kukiuka mkataba.
Mashabiki wengi wamekuwa wakielezea hasira yao shisi ya Ronaldo kwenye mitandao ya habari ya kijamii.
"Amesaliti mashabiki 60,000 na kutudharau," alisema mmoja wa mashabiki waliokuja kutazma mechi hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
0 comments:
Post a Comment