Nyota
wa klabu ya Manchester City, Raheem Sterling amefunguka mazito kuhusu
maisha aliyopitia wakati alipokuwa na umri mdogo, kuhusiana na kifo cha
baba yake mzazi, kuchapwa na mkanda shuleni alipokuwa Jamaica na namna
kocha wake Pep Guardiola alivyomtia moyo ndani ya timu hiyo ya
Uingereza.
Mshambuliaji huyo wa mabingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza, Sterling ameyasema hayo wakati ambapo picha zake zinatarajiwa kutumiwa katika ukurasa wa mbele jarida la August’s edition of GQ magazine litakaloanza kupatikana siku ya Ijumaa.
Kwenye
jarida hilo, Sterling ataonekana akiwa na mabawa mgongoni huku akiwa
amevalia suruali nyeusi. Kwenye mahojiano hayo staa huyo alikuwa karibu
kabisa na baadhi ya wachezaji wa timu yake.
Mbali
na picha hizo kumuonyesha Sterling mwenye umri wa miaka 24 akiwa na
mbawa kubwa za rangi nyeusi mgongoni na kuvalia ‘combat’ nyeusi,
‘bracelet’, saa lakini pia ameonekana akiwa cheni kubwa inayozunguka
maeneo ya shingo yake wakati akiwa tumbo wazi.
Sterling
ameishi Jamaica huku akiwa bila ya baba baada ya kuuawa wakati akiwa na
umri wa miaka miwili pekee kisha miaka mitatu baadae ndipo akahamia
jijini London.
Baba mzazi wa Raheem Sterling, Phillip Slater picha ikiwa imepigwa mwaka 1996 alipokuwa na miaka 29
Ameliambia jarida la GQ kuwa wakati mwingine ni vigumu lakini kila kitu hutokea kwa sababu maalumu, “Wakati mwingine ni vigumu lakini kila kitu hutokea kwa sababu.”
Ameliambia jarida la GQ kuwa wakati mwingine ni vigumu lakini kila kitu hutokea kwa sababu maalumu, “Wakati mwingine ni vigumu lakini kila kitu hutokea kwa sababu.”
“Kwa
sasa nina wangu, nitahakikisha nawapatia mapenzi kutoka kwa baba yao
ambayo mimi mwenye sikuwahi kuyapata. Na nafikiri nitajiskia furaha hata
na mimi mwenyewe.” – Amesema Sterling.
“Kwa
maa ya kwanza iliniwia ugumu, kama unavyofahamu shule ni kitu cha
tofauti. Hapa kuna shule nyingi lakini wakati nilipokuwa Jamaica ni
tofauti na uvumilivu ni sifuri.”
“Nafikiri
Serikali ya kule ndiyo iliyokuwa ikichangia, kunawakati ukatili ulikuwa
umezidi mashuleni.” Sterling na mpenzi wake, Paige Milian wamekuwa
katika mahusiano kwa muda mrefu na kujaaliwa kuwa na watoto wawili ambao
ni Thiago, two, na Melody Rose, seven.
Sterling akiwa na familia yake, mpenzi wake Paige Milian na watoto wao Thiago, two, na Melody Rose, seven
Sterling
amekuwa katika kipindi kizuri sana kwenye nafasi yake ya ushambuliaji
na kuisaidia klabu ya Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini
Uingereza akiwa chini ya kocha Pep Guardiola.
Akimzungumzi
kocha huyo, Sterling amesema amekuwa na mahusiano mazuri naye “Mara
kadhaa amekuwa akinipatia changamoto, amekuwa haniachi hata ni pumzike,
kila mwaka amekuwa akisajili mchezaji ambaye anacheza nafasi yangu.”
0 comments:
Post a Comment