Home
»
»Unlabelled
» Samatta aandika ujumbe huu kwa Watanzania “Hili lilikuwa darasa tosha kwetu sote, Ulikuwa ni wakati wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake kujifunza kitu”
Wakati
michuano ya Afcon ikiendelea nchini Misri huku Tanzania ikitolewa
mapema kwenye makunbdi baada ya kupoteza michezo yote mitatu Nahodha wa
Tanzania Mbwana Ally Samatta ameamua kuandika ujumbe huu kwa Watanzania: Tanzania’s
forward Mbwana Samatta (R) is marked by Algeria’s defender Mehdi Tahrat
during the 2019 Africa Cup of Nations (CAN) Group C football match
between Tanzania and Algeria at the Al Salam Stadium in the Egyptian
capital Cairo on July 1, 2019. (Photo by JAVIER SORIANO / AFP)“Ilikuwa ni ndoto ya kila mtanzania kuona tunashiriki michuano ya #AFCON na
sote tulifurahia kupata nafasi hii. Tunafahamu watanzania walitamani
timu ifanye vizuri na kufika mbali, hata sisi wachezaji hilo lilikuwa
lengo letu namba moja lakini hali halisi imefuta ndoto zetu. Tunawashukuru
mashabiki wote mliotuunga mkono katika kipindi chote kuanzia maandalizi
hadi leo, nawaomba mfahamu tu kuwa hili lilikuwa darasa tosha kwetu
sote. Ulikuwa ni wakati wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake kujifunza
kitu. Tuendelee kushikamana. HAINA KUFELI”
By Ally Juma.
0 comments:
Post a Comment