Baada ya Simba SC Salamba atua timu hii Bongo
Mchezaji wa Simba SC, Adam Salamba amefanikiwa kujiunga kwa mkopo na timu yake mpya Namungo FC inayojiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Salamba amejiunga na kikosi hicho kwa mkopo wa mwaka mmoja, lakini alishindwa kujiunga na wenzake kutokana na kwenda Afrika Kusini katika majaribio ambayo hayakufanikiwa.
Mwenyekiti wa Namungo FC, Hasani Zidadu amesema walimyakua mchezaji huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa, lakini walimuacha kutokana kuwa na mambo mengine binafsi.
0 comments:
Post a Comment