Monday, August 12, 2019



PEP Guardiola, Meneja wa Manchester City amesema kuwa mfumo wa sasa wa komputya wa VAR unaua utamu wa soka halisi la awali.

City imeanza kutupa kete yake ya kwanza vema kwenye mechi za Ligi Kuu England wakiwa ni mabingwa watetezi baada ya kuifunga mabao 5-0 West Ham United na mfumo wa VAR umeanza kutumika.

"Huu si mfumo bora kwani unaua kabisa utamu wa soka halisi ambalo tumelizoea hapo awali, mchezaji na shabiki hana uhuru wa kushangilia bao mpaka kompyuta iseme.

"Naona si jambo nzuri afadhali soka lingebaki mikononi mwa waamuzi pekee na si kama livyo sasa," amesema.

0 comments:

Post a Comment