Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo'
amesema kuwa bajeti ya klabu hiyo katika msimu wa 2019/20 itakuwa mara
mbili na nusu ya msimu uliopita.
Akifanya mahojiano na Shirika la Habari nchini Uingereza BBC, Mo amesema
kuwa ameyaona mabadiliko makubwa ndani ya kipindi cha msimu mmoja, kitu
ambacho kinamfanya azidi kuwa nguvu ya kuwekeza zaidi ili kufukia
kuwa klabu kubwa Afrika.
"Miaka mitano iliyopita, watu walipoteza kabisa matumaini ya kufuatilia
klabu na wengi wao walikimbilia kuangali Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza,
hakuna ambaye alikuwa na habari na Simba", amesema.
"Ndio maana mwaka uliopita tuliweka nguvu kubwa zaidi, tukawaleta
wachezaji wakubwa wa Kimataifa, tukatengeneza mfumo wa kusaka wachezaji
'Scouting' pamoja na kumpata kocha mkubwa. Bajeti yetu ya msimu uliopita
hadi msimu huu imeongezeka mara mbili na nusu", ameongeza.
Aidha Mo Dewji amesema kuwa alitumia fursa ya kukuza kurasa za mitandao
ya kijamii za klabu ya Simba kuwa za kiweledi zaidi pamoja na
kuzirasimisha baada ya kuona kwamba Watanzania wengi wanafuatili
mitandao ya kijamii, ambapo amesema hatua hiyo imeifanya klabu kukua
mara dufu ndani na nje ya nchi.
Home
»
»Unlabelled
» Mo Dewji Ataja Bajeti ya Simba Msimu wa 2019/20
Tuesday, August 13, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment