Tuesday, August 13, 2019


Bosi wa klabu ya Barcelona amesafiri kuelekea nchini Ufaransa kwaajili ya kufanya mazungumzo na klabu ya Paris Saint-Germain ili kumrudisha Camp Nou Mbrazil, Neymar.
Image result for neymar to barcelona
Mkurugenzi huyo wa miamba ya soka ya Hispania, Eric Abidal amekwea pipa hadi jijini Paris ili kumrejesha staa huyo kwa mabingwa wa La Liga.
Mpaka sasa Neymar ametumia misimu minne nchini Hispania akiwa sambamba na mastaa wengine Lionel Messi na Luis Suarez huku wakifanikiwa kushinda makombe mawili ya Ligi pamoja na Champions League mwaka 2015 wakiwa pamoja.
Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Santos amecheza jumla ya michezo 185 na kufanikiwa kufunga mabao 101 nchini Hispania.
Kwa sasa mashabiki wa PSG wamekuwa wakionyesha hisia zao kwa kumtaka Neymar kuondoka wakati wa mchezo wao wa ufunguzi wakifunga 3-0 wa Ligue 1 dhidi ya Nimes.
Mchezaji huyo ghali zaidi duniani, Neymar aliondoka Barcelona kwenda PSG kwa usajili uliyoweka rekodi wa euro milioni 200 mwaka 2017 wakati mpaka sasa akiwa amefunga jumla ya mabao 51 kati ya michezo 58  aliyocheza kwa mabingwa hao wa Ligue 1.

0 comments:

Post a Comment