The Sun imeripoti kuwa Rooney amekuwa akiishi Marekani na familia yake tangu mwaka uliopita, lakini tayari mkewe ameondoka huko na kurudi Uingereza kutokana na vituko vya ulevi vinavyoendelea.
Wakati uhusiano wake na mkewe umekuwa wa mashaka kutokana na matukio mbali mbali ya ulevi wa Rooney. Mapema mwaka huu alikamatwa na polisi kwa kulewa kupita kiasi akiwa uwanja wa ndege Marekani.
Kwa mujibu wa jarida la Mirror, Rooney anatarajiwa kurudi Uingereza mwezi Oktoba na yupo tayari kujiunga na Derby ya nchini humo ili kutumia fursa ya kuwa karibu na mkewe ambapo pia atakutana na mtu wa ushauri nasaha ili kurejesha amani katika ndoa yake.
Inasemekana maamuzi ya Rooney kurudi Uingereza yatamgharimu mamilioni ya pesa. Lakini mkewe alitaka Rooney ampe kipaumbele yeye Coleen na watoto.
Hivyo Rooney ameamua kufanyia kazi hilo “si tatizo kupoteza pesa kwani ni thamani zaidi kumfanya Coleen awe na furaha”
0 comments:
Post a Comment