MEDDIE
Kagere mshambuliaji wa Simba, ametoa tahadhari kwa wachezaji wenzake
akisema kwamba hawatakiwi kuwachukulia kirahisi wapinzani wao UD do
Songo.
Simba
itamenyana na UD Songo kwenye mchezo wa marudio kati ya Agosti 23-25
jijini Dar baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa
kwanza uliochezwa nchini Msumbiji.
Msimu
uliopita kwenye michuano ya kimataifa, Kagere alitupia mabao sita ana
kazi ya kufanya pamoja na wachezaji wake kwenye mchezo wa marudio ili
kusonga mbele.
“Kuelekea
mchezo wa marudio tunatakiwa kuwa makini na kuchukulia kwa uzito mkubwa
pambano ambalo tutachezwa kwani mashabiki pamoja na uongozi unahitaji
matokeo," amesema.
0 comments:
Post a Comment