Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, amesema kuwa bado hajajua wachezaji wa Yanga ambao hawajajiunga na kikosi watarejea lini kwa sasa.
Juma Abdul na Andrew Vincent 'Dante' hawakujiunga na kikosi kambini Morogoro hata timu ilipojichimbia Visiwani Zanzibar hawakugusa kambini kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa wanadai stahiki zao.
Habari zinaeleza kuwa beki kisiki, Kelvin Yodani yeye amejiunga na timu ila sharti lake ni moja kama ilivyo kwa wenzake kwamba ni lazima alipwe stahiki zake zote.
Mwakalebela amesema kuwa:"Kwa sasa sijajua wachezaji hao watarejea lini kambini kwa kuwa wao ndio walianza kugoma,
"Ni wachezaji muhimu na mchango wao ni mkubwa kama ambavyo walipambana msimu uliopita ila kwa sasa uongozi tutakaa ili kumaliza matatizo haya," amesema.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.