Pambano la
marudiano kati ya Andy Ruiz Jr na Anthony Joshua litafanyika mwezi
Disemba nchini Saudi Arabia, promota wa Joshua Eddie Hearn
amethibitisha.
Kumekuwa na tetesi kuwa Ruiz Jr hayupo tayari kwa
pambano hilo, lakini Hearn amesema kuwa mabondia wote wawili wameshaini
kucheza mpambano huo Disemba 7 mwaka huu.Ruiz aliushangaza ulimwengu wa masumbwi kwa kumchakaza Joshua mwezi Juni na kutawazwa kuwa bingwa wa dunia.
Bingwa huyo mpaka sasa hajawaarifu chochote mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na mpambano huo wa marejeano toka ulipotangazwa siku ya Ijumaa.
Mkufunzi wake, Manny Robles amesema "kuna sababu inayommfanya" Ruiz kukaa kimya.
- Tetetesi za soka Ulaya Jumanne 13.08.2019
- 'Neymar akaribia kuihama PSG'- Je anaelekea wapi?
- Makonda kukabiliana na wanaume walaghai wa mapenzi
Katika mkutano na wanahabari, ambao hata hivyo si Joshua wala Ruiz ambaye alihudhuria, Hearn alitangaza kuwa mpambano huo utafanyika katika uwanja wa wazi katika kitongozji cha Diriyah, nje kidogo ya jiji la Riyadh.
Omar Khalil, ambaye anafanya kazi na Serikali ya Saudia katika kuandaa pambano hilo pia ametangaza kuwa wote watakaonunua tiketi za mpambano huo moja kwa moja watakuwa wamepewa viza ya kuingia nchini humo.
Upande wa Ruiz uliweka wazi kuwa usingekubali kucheza pambano la marejeano nchini Uingereza huku upande wa Joshua ukitaka pambano hilo lichezwe nje ya Marekani.
"Tulipata ofa kutoka Saudi Arabia, Abu Dhabi, Dubai na Qatar," aliongezea Hearn. "Tulitaka kwenda sehemu ambayo wana maono ya mbali na mchezo wa masumbi. Tulijua Saudia inamaanisha na imewkeza kwenye mchezo huu."
"Inabidi tutambue kuna ulimwengu mwengine nje ya Uwanja wa Cardiff na Madison Square Garden. Tunalazimika kukuza mchezo huu katika maeneo mengine duniani.
Ruiz, alimpoka Joshua mikanda ya IBF, WBA na WBO Juni mosi baada ya kumuangusha mara nne kabla ya mpambano huo kukatishwa na mwamuzi.
Mkataba unamlazimisha kucheza pambano la marudiano, na awali idhaniwa kwa ukimya wake labda hajasaini pambano hilo.
Kuna wanaodhani kuwa ukimya wa Ruiz unatokana na kudai kitita kikubwa zaidi ya alichopewa awali.
Pambano hilo linatarajiwa kuingiza pesa nyingi, mpaka sasa inaarifiwa kuwa waandaaji nchini Saudia wametoa dola milioni 40, na bado hapo kuna kitita cha watakaolipia watazamaji kwenye runinga hakijajumuishwa.
Waandaaji nchini Saudia wanasema nchini mwao kuna hamu kubwa ya matukio kama hayo kutokana na uhalisia kuwa 70% ya wananchi milioni 40 ni vijana chini ya miaka 24.
Hata hivyo, makundi ya kutetea haki za binaadamu yanapinga vikali kuandaiwa kwa mapando ya ukubwa wa kiasi hicho nchini humo.
Wanadai kuwa matamasha ya michezo na burudani yanatumika na serikali ya kifalme kuonesha kuwa nchi hiyo imebadilika na kuwa ya kisasa ilhali haki za binaadamu zinaendelea kuvunjwa kila uchao.
0 comments:
Post a Comment