Tuesday, August 13, 2019


Staa mpya wa club ya Real Madrid ya Hispainia Eden Hazard aliyejiunga na timu hiyo akitokea Chelsea ya England, hatimae amekabidhiwa jezi namba 7 ndani ya club ya Real Madrid baada ya ombi lake kwa Luka Modric kuomba amuachie jezi namba 10 kugonga mwamba.

Hazard anapewa jezi namba 7 ambayo ilikuwa ikitumiwa na Cristiano Ronaldo aliyepo Juventus kwa sasa na Raul Gonzalez enzi anacheza timu hiyo, baada ya kuondoka Ronaldo jezi namba saba ndani ya Real Madrid alipewa Mariano Diaz.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki katika mtandao wa twitter hawakubaliani na kupewa jezi namba saba kwa Eden Hazard kwani atakuwa analinganishwa na Cristiano Ronaldo, kitu ambacho anaweza kushindwa kufikia kiwango au makubwa ya Ronaldo yaliofanywa katika timu hiyo, katika michezo ya maandalizi ya msimu Hazard alikuwa akivaa jezi namba 50.



0 comments:

Post a Comment