Tuesday, August 13, 2019

 
Serena Williams Aubwaga Ubigwa kwa Chipukizi wa Canada
Mchezaji mahiri wa tenisi ambaye ni raia wa Marekani, Serena Williams mwenye umri wa miaka 38 amepoteza nafasi ya kushinda Kombe la Rogers.

Kwa mujibu wa CNN, Serena alilazimika kusitisha mchezo wa fainali hiyo akiwa mjini Toronto dhidi ya chipukizi Bianca Andreescu wa Canada baada ya kupata tatizo la misuli.

Bianca Andreescum mwenye umri wa miaka 19 amekuwa raia wa kwanza wa Canada aliyetwaa ubingwa wa Kombe la Rogers  kwa wanawake tangu mwaka 1969.

Chipukizi  huyo amepokea ubigwa huo akibubujikwa na machozi  akionesha kumuonea huruma Serena kwa maumivu aliyoyapata. Ni dhahiri angependa apewe ubingwa baada ya kushinda kwa kuonesha uwezo kuliko hali ilivyokuwa.

“Unanifanya nilie, najua ni jinsi gani inauma kujitoa kwenye mashindano,” alisema Bianca akiwa anamfariji Serena aliyeonekana kuumizwa na tukio hilo.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Serena William kujitoa kwenye mashindano ya Kombe la Rogers kwa sababu ya majeraha ni mwaka 2000, mwaka ambao Bianca alizaliwa.

0 comments:

Post a Comment