Friday, January 28, 2022

 



TIMU ya Dodoma Jiji FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Sumbawanga United usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na Khamis Mcha mawili, moja kwa penalti dakika ya tisa na lingine dakika ya 22, wakati mengine yamefungwa na Seif Abdallah Karihe dakika ya 30 na Anuary Jabir dakika ya 80.
Mechi nyingine za 32 Bora michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Polisi Tanzania imeitoa Ndanda FC kwa kuichapa 3-1, wakati Bagamoyo Friends imeitoa Catamine kwa kuichapa 2-1.

0 comments:

Post a Comment