Thursday, August 1, 2019

Manchester United bado hawajaamua kuhusu suala la kuhama kwa Paulo Dybala
Image caption Manchester United bado hawajaamua kuhusu suala la kuhama kwa Paulo Dybala
Manchester United bado hawajaamua kuhusu suala la kuhama kwa Paulo Dybala, huku mshambuliaji huyo wa Argentina , 25, akitarajia kujadili na Juventus juu ya hali yake ya baadae wiki hii . (Manchester Evening News)
Dybala ameiambia klabu ya United kuwa itatakiwa kumpa mkataba wenye thamani ya pauni £350,000 kila wiki ikiwa atakiunga nao. (Mail)
Rais wa kblabu ya Lille Gerard Lopez amethibitisha kuwa winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa Arsenal kwa euro milioni 80. (RMC Sport - in French)
  Winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa Arsenal
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa Arsenal
Napoli wamejipanga kwa dau la Euro milioni 60 kwa ajili ya winga wa Crystal Palace na mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha baada ya kumkosa Pepe. (Mail)
Barcelona wanataka kumuuza Mbrazili Philippe Coutinho, lakini wanahofia kuwa kuwa hawajapata ofa yoyote kumuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 . (ESPN)
Arsenal imetengeneza dau la deni la mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani mwenye umri wa miaka 25 kwa ajili ya kuwa nae kwa misimu miwili. (Gazzetta dello Sport, via Sun)
Nahodha Laurent Koscielny, mwenye umri wa miaka 33, bado ameazimia kuondoka Arsenal msimu huu licha ya mazungumzo yanayoendelea baina yake na klabu hiyo.(Independent)
 
Arsenal imetengeneza dau la deni la mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani
Image caption Arsenal imetengeneza dau la deni la mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani
Arsenal wamejiandaa kumuacha mlinzi wao Mjerumani Shkodran Mustafi aondoke msimu huu, lakini Roma abado hawaweka dau kwa ajili yake licha ya kwamba wanahusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.(Romanews, via Star)
Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic anasema kuwa Manchester City wanapaswa kuombwa msamaha baada ya meneja wa klabu Niko Kovac kusema kuwa timu hiyo ya Ligi ya Bundesliga imejipanga kusaini mkataba na winga wa Mjerumani Leroy Sanes mwanye umri wa miaka 23. (Sport Bild - in German)
Zenit St Petersburg wanatarajia kutangaza kusaini mkataba wa winga wa Barcelona Malcolm, mwenye umri wa miaka 22,baada ya klabu mbili kukubaliana kuhusu garamakatika kanda hiyo ya £36.5m na zaidi kwa ajili ya Mbrazili huyo. (Goal)
  Aston Villa ya wanamsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal Maupay
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aston Villa ya wanamsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal Maupay
Manchester United wako tayari kukabiliana na Barcelona katika kumpata mshambuliaji wa klabu ya Marseille mwenye umri wa miaka 17 Mfaransa Lihadji msimu huu. (La Provence, via Mail)
Nia ya Aston Villa ya kumsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal Maupay imeongezeka zaidi baada ya Sheffield United kutafuta katika timu nyingine . (Birmingham Mail)
Sunderland watamrugusu kiungo wao wa kati na nahodha captain George Honeyman, mwenye umri wa miaka 24, kujiunga na kikosi cha Hull Citybadala ya kumkosa mhitimu wa shule ya soka kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Northern Echo)
Mchezaji mwenza wa Neymar katika kikosi cha Paris St-Germain Marco Verratti anakiri kuwa klabu hiyo lazima imuuze mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27- raia wa Brazil ikiwa hana raha katika Parc des Princes, licha ya kocha Thomas Tuchel wa kutaka mchezaji huyo abaki kikosini. (Express)
  Real Madrid wamemuambia mshambuliaji wa safu ya kati wa MColombia James Rodriguez kuwa atabaki Bernabeu
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Real Madrid wamemuambia mshambuliaji wa safu ya kati wa MColombia James Rodriguez kuwa atabaki Bernabeu
Juventus amethibitisha kuwa kumekuwa na ofa kwa ajili ya mshambuliaji wake raia wa Argentina Paulo Dybala, huku kukiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo kutoka kwa Manchester United na Tottenham ya kumnunua . (Mirror)
Mlinzi wa zamani wa Barcelona Carles Puyol, mwenye umri wa miaka 41, amesema kuwa alikataa mara mbili ombi la Real Madrid la kutaka ajiunge nao. (AS in Spanish)
Meneja wa Rangers Steven Gerrard amethibitisha kuwa uhamisho wa winga wa Liverpool Muingereza Ryan Kent, ambaye ana umri wa miaka 22, haupo na kwamba hawawezi kumudu uhamisho wake kudumu . (Daily Record)

0 comments:

Post a Comment