
Manchester City
wamekataa dau la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili
ya mshambuliaji wa Leroy Sane raia wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka
23. (Metro)
City wanataka walipwe pauni milioni 137 kwa mauzo ya
Sane ikiwa hatakuwa na haja ya kusaini mkataba wa kurefusha mkataba
wake, unaomalizika Juni 2021. (Telegraph)
Manchester United wanahangaika kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, na muwakilishi wake, na hivyo kuuweka hatarini mkataba na Juventus wa kubadilishana mchezaji wa safu ya mashambulizi Mbelgiji Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26. (Independent)
Mlizi wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, ameachwa nje ya kikosi cha Leicester kitakachocheza mechi ya urafiki baina yao na Atalanta Ijumaa kutokana na hali ya sintohfahamu juu ya hali ya yake ya baadae na Foxes wanaotaka mkataba wa pauni milioni 90 ikiwa Manchester United wanasaini mkataba nae. (Telegraph)
- Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi tarehe 01.08.2019
- Arsenal imethibitisha kumsaini Nicholas Pepe kwa £72m
- Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 31.07.2019
Manchester United ilikataa fursa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 19 Moise Kean, na kumruhusu mtaliano huyo kuwa huru kuhamia Everton. (90min)


Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 30.07.2019
Betis wamekataa ofa kadhaa kutoka kwa Tottenham kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Lo Celso. (SevillaABC - in Spanish)
Kiungo wa kati- nyuma wa Argentina Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31, anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu hiyo.(Sun)
Mchezaji wa safu ya nyuma-kushoto wa Brazil Dani Alves anakaribia kuhamia Sao Paulo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 36- yuko huru baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Goal)
Crystal Palace wamefany amawasiliano na Cardiff City kumuhusu kiungo wa kati wa Real Betis Muhispania Victor Camarasa mwenye umri wa miaka 25
0 comments:
Post a Comment