Friday, August 2, 2019


KLABU ya Arsenal yenye maskani yake kaskazini mwa London nchini uingereza imeweza kumnasa winga kutoka Lille ya Ufaransa, Nicolas Pepe.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ivory Coast ameweza kunaswa kwa ada ya paundi za kiingereza 72.9 million ambapo zimeweza kuwa record ya klabu kwenye manunuzi ya mchezaji, msimu uliopita Arsenal walitumia paundi 55 million za kiingereza kuipata saini ya Pierre-Emerick Aubameyang kutokea Dortmund.
Nicolas pepe mwenye umri wa miaka 24 ameweza kujiunga na arsenal akitokea lille ya ufaransa  na kusaini kwa washika bunduki mkataba wa miaka mitano.

0 comments:

Post a Comment