Maono yake makubwa alikuwa anataka kuja kuwa padre lakini ghafla amejikuta yupo kwenye mpira.
Huyu hapa anafunguka mengi alizungumza na Saleh Jembe:-
"Soka nilianza mwaka 2017, nilikuwa nataka kuwa padre mambo yakaingiliana nikaenda kusoma masuala ya afya kwenye chuo kimoja hivi huko Sengerema.
Umeanza lini kujihusisha na soka?
"2017 nilianza kutumikia timu ya utumishi FC, Meatu Shinyanga hapa ilikuwa ni sehemu ambayo najifunza tu mpira.
"Nilikuwa nacheza bila malipo na Joseph Chale, mwalimu wa Chuo alinifuata na kuniambia ninajua mpira hivyo inabidi unilipe.
Ndugu zako walikubali ucheze mpira?
"Baba alikuwa hatakati nicheze mpira ila mama alimshawishi baadaye akaelewa. Kuna academy moja nilikuwa najifunza na nikapata dili la kufanya mazoezi ndani ya Simba b, kabla sijaenda Simba nikadakwa na Yanga,
Ulikuwa unafanya mazoezi na nani?
"Anthony Chibase, Mohamed Mposso kocha wa makipa hawa ndio walikuwa wananifundisha kazi na nimefanya nao kwa ukaribu.
Ulipewa kandarasi ya muda gani?
"Sikupata mkataba nilikuwa ndani kwa muda wa wiki tatu, Kakolanya, Rostand na Kabwili,hawa nimefanya nao kazi chini ya Pondamali ambaye alinielewa, Beno Kakolanya alikuwa ananirekebisha makosa yangu mengi. Pia Shadrack Nsajigwa alikuwa ananielewa.
Uliondoka lini Yanga?
"2018 mwezi wa sita niliachana na Yanga nikaenda kufanya trial Coastal Union nako nikaaona mambo magumu kwani nafasi nilipata ila sikutangazwa.
"Nikatimkia Mwadui kwa kocha Binzimungu msimu wa 2018-19 nikajiunga na Mwadui FC
"Mechi ya Kwanza ilikuwa dhidi ya Biashara United tulipata ushindi wa mabao 2-0
"Mechi ya tatu dhidi ya Mbeya City nilipoteza na Ambokile alikuwa wa Kwanza kunifunga. Nimecheza jumla ya mechi 27 clean sheet 10, kupoteza 6, Sare 11.
"Klabu ambazo zilikuwa zinanihitaji ni, Namungo, Polisi Tanzania, Kagera na shida ilikuwa maelawano," anamalizia Mbisse ambaye ana mkataba wa miaka miwili ndani ya Mwadui FC.
0 comments:
Post a Comment