Wednesday, August 14, 2019



UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umejipanga kwafuata wapinzani wao Township Rollers kishujaa kwa kuongeza majembe matatu ya kazi.

Makamu Mwnyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wanatarajia kupata leseni kutoka kwa Caf ili kuwatumia wachezaji wake watatu ambao hawakucheza mchezo wa awali Dar.

"Tunatarajia kuwafuata Rollers tukiwa kamili kwa sasa tunasubiri barua kutoka Caf ambayo itatupatia leseni kwa wachezaji wetu muhimu watatu.

"Sababu kubwa ya haya kutokea ni kuwahi kuanza kwa michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani hata Azam FC na KMC pia wamekubwa na hili," amesema

Katika hatua nyingine Mwakalebela amesema wamefanya mawasiliano na CAF na wanatarajia kupata leseni za wachezaji wao watatu kabla ya kwenda Botswana," amesema.

Wachezaji ambao hawana leseni ya Caf ni pamoja na Farouk Shikalo, David Molinga 'Falcao' na Moustafa Seleman, chezo huo Yanga ina kibarua cha kutafuta ushindi baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1, na mfungaji akiwa ni Patrick Sibomana.

0 comments:

Post a Comment