Manchester
United ina mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark
Christian Eriksen, 27, mwezi Januari mwakani kwa bei iliopunguzwa
kandarasi yake ikiingia mwaka wa mwisho katika klabu hiyo .(Sun) United
itamenyana na Inter Milan kupata saini ya Eriksen. (Express)
ottenham inataka kumsaini mchezaji wa Fulham wa chini ya miaka -20 Steven Sessegnon, ambaye ana uwezo wa kucheza safu ya ulinzi na ya kati – mwezi mmoja baada ya kumsaini pacha wake Ryan kwa £25m. (Sun)
Winga wa Chelsear Willian, 31, ananyatiwa na kocha wake wa zamani Maurizio Sarri ambaye sasa ni mkufunzi wa Juventus, wakati kandarasi ya nyota huyo Stamford Bridge ikiingia mwaka wa mwisho . (Express)
Liverpool inamnyatia kipa wa Trabzonspor mabaye bei yake inakadiriwa kuwa £14m- Ugurcan Cakir. Reds walifuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki wa miaka 23- wakati wa timu yake ilipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Fenerbahce wikendi iliopita. (Mail)
Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, ambaye atatimiza miaka 70 mwezi ujao, anataka kurejea katika wadhifa wa usimamizi – miezi 16 baada ya raia huyo wa Ufaransa kuacha kazi kama kocha wa Gunners kwa karibu miaka 22. (Sun)
Liverpool na Chelsea wanapania kumsajili mshambuliaji wa Wigan Athletic wa miaka 17- Muingereza Joe Gelhardt, ambaye ameshirikishwa mara tatu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Mirror)
Jaribio la Bayern Munich kumsajili winga wa Manchester City Leroy Sane, 23, msimu wa juto limetibuka baada ya kushindwa kufikia masharti ya mshahara wa mchezaji huyo. (Manchester Evening News)
Beki wa kulia wa England Kieran Trippier, 28, amesema kujiunga na Atletico Madrid kutoka Tottenham mwezi Julai ilikua “hatua kubwa”. (Diario AS – in Spanish)
Mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling, ambaye awali alijiunga na Roma kwa mkopo huenda akasalia katika klabu hiyo ya Italia zidi ya msimu huu. (Manchester Evening News)
mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa akidai kuwa amekataa ofa ya vilabu kadhaa vilivyotaka kumsajili. (mail)
Juventus imewaondoa wachezaji Emre Can, 25,wa wa Ujerumani, mshambuliaji wa zamani wa Croatia Mario Mandzukic, 33, na beki wa Italia Giorgio Chiellini,35, katika kikosi chake cha mwaka wa 2019-20 cha Champions League awamu ya makundi. (Football Italia)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage caption
0 comments:
Post a Comment