Cristiano
Ronaldo amezidi kujiwekea historia baada ya kutwaa tuzo ya 10 kama
mchezaji bora wa mwaka nchini Ureno. Hii ikiwa ya pili kunyakuwa katika
siku za hivi karibuni baada ya ile ya Marca’s Legend award kutoka Hispania.
Ronaldo
mwenye umri wa miaka 34, amekuwa akifanya vizuri kwenye tuzo hizo tangu
mwaka 2007. Huku akiisaidia klabu yake ya Juventus kutwaa taji la nane
mfululizo la Serie A.
Nyota huyo
ametwaa tuzo hiyo kwa kumshinda kinda wa Atletico Madrid, Joao Felix,
mchezaji wa Manchester City, Bernardo Silva, kiungo wa Sporting Lisbon,
Bruno Fernandes na Ruben Neves wa Wolves.
Amekuwa akishinda tuzo hiyo mfululizo tangu 2007 waka mwaka 2010 na 2014 ndiyo kipindi pekee ambacho hakuchukua. Kwa sasa anaongoza akichukua mara 10 akifuatiwa na Luis Figo aliyechukua mara sita (6) pekee.
Tuzo
hizo zimetolewa huko Carlos Lopes Pavilion katika jiji la Lisbon mahala
ambapo Ronaldo amekulia wakati alivyokuwa kijana mdogo. Mchezaji huyo
alipata nafasi ya kuzungumza mara baada ya kuchukua tuzo hiyo.
“Huu
ulimwengu unakwenda kasi sana, watu wengi wamekuwa bize katika mitandao
ya kijamii. Imekuwa ni mwaka mgumu sana kwa mtu mmoja mmoja, lakini
usikubali mtu yoyote akukatisha tamaa. Sina msada lakini naweza kusema
Sporting inastahili zawadi hata kidogo, muda ujao.” Cristiano RonaldoWashandi mbalimbali wa tuzo hizo za Ureno
Mchezaji bora wa mwaka wa kiume: Cristiano Ronaldo (Juventus)
Mchezaji bora wa mwaka wa kike : Jessica Silva (Levante / Lyon)
Kocha bora wa mwaka wa kiume : Bruno Lage (Benfica)
Kocha bora wa mwaka wa kike : Miguel Santos (Braga)
Timu bora kwa upande wa wamaume tuzo imekwenda kwa : Benfica
Timu bora kwa upande wa wanawake imekwenda kwa : Benfica
0 comments:
Post a Comment