Wednesday, October 9, 2019


Club ya AC Milan ya Italia usiku wa October 8 2019 imefikia maamuzi mazito ya kumfuta kazi kocha wao mkuu Marco Giampaolo baada ya kuifundisha timu hiyo katika michezo saba pekee.
AC Milan wamefikia maamuzi hayo ya kumfuta kazi Marco baada ya club yao kuendelea kuwa katika hali mbaya Serie A na kuwa katika mwenendo usioridhisha toka kocha huyo alipomrithi Gennaro Gattuso mwezi June
Katika mechi 7 Marco Giampaolo alizoziongoza chini ya AC Milan katika Serie A ameshinda michezo mitatu na kupoteza minne huku timu ikiwa nafasi ya 13 kwa kuwa na point 9 lakini ni point 3 dhidi ya timu zilizopo katika nafasi za kushuka daraja.

0 comments:

Post a Comment