Thursday, October 17, 2019



Rais wa klabu ya Zamalek, Mortada Mansour ameongeza sheria mpya katika utawala wake, kwa kuwapiga marufuku wachezaji wa klabu hiyo kutumia mitandano ya kijamii.

Raisi huyo  ambaye pia ni mbobezi wa maswala ya sheria, amepiga marufuku ya mitandao ya kijamii kwa kuamini wachezaji wengine wamekua wakipoteza muda mwingi kwa matumizi ya simu.

Mchezaji yeyote wa Zamalek atakayebainika anamiliki akaunti ya kijamii atakatwa nusu ya mshahara wake, huku kukiwa na faini ya dola 18,00 za kimarekani kwa kila post itakayowekwa na mchezaji kwenye mtandao wa kijamii.

Mitandao ya kijamii inaonekana kuwa na athari kubwa kwa wachezaji kwani si Afrika pekee bali hata England, meneja wa Man City Pep Guardiola amekuwa mpingaji mkubwa wa matumizi ya simu kwa wachezaji na aliitambulisha sheria mpya mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment