Wednesday, October 9, 2019



Imeelezwa kuwa aliyekuwa CEO wa klabu ya Simba, Crescentius Magori amekanusha taarifa ambazo zimesambaa katika mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya wachezaji wa timu hiuo kugoma.

Taarifa zilizosambaa awali zilieleza kuwa baadhi ya wachezaji wa Simba waligoma na sababu zikitajwa kuwa wanaidai fedha zao za usajili.

Kufuatia kusambaa kwa taarifa ikiwemo kupitia kituo kimoja cha Radio hapa nchini, Magori ameibuka na kusema atalifikisha suala hilo katika vyombo vya sheria kwakuwa linaidhalilisha klabu.


Taarifa imesema kuwa Magori atafika katika vyombo vya sheria ikiwemo kukishtaki chombo kilichohusiaka na kusambaza taarifa hizo ambazi si za ukweli.

0 comments:

Post a Comment