UONGOZI wa Singida United umesema kuwa utatumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mkoani Arusha kwenye mechi zao mbili za nyumbani za ligi kuu bara dhidi ya Simba na JKT Tanzania.
Singida United ilikuwa inatumia uwanja wa Namfua ambao kwa sasa umefungiwa na Bodi ya Ligi Tanzania ili ufanyiwe maboresho.
Festo Sanga Katibu Mkuu wa Singida United amesema kwa sasa wanafanyia marekebisho uwanja wa Namfua kisha watarejea kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Mchezo wa Simba utachezwa Oktoba 27 na ule wa JKT Tanzania utapigwa Oktoba 30.
0 comments:
Post a Comment