Monday, October 14, 2019


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ Khalfan Majani, ameibuka mfungaji bora katika mashindano ya timu za taifa kwa Bara la Afrika yajulikanayo kama CANAF, yaliyokua yakifanyika nchini Angola.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ Khalfan Majani
Majani, amefunga magoli sita katika michezo sita, huku pia akiiwezesha Tembo warriors kuwa kati ya timu nne zilizokata tiketi ya kufuzu kucheza michuano ya kombe la Dunia kwa wenye ulemavu mwaka 2022.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ Khalfan Majani
Ikumbukwe kwamba Majani pia ndiye mchezaji pekee aliyefanikiwa kufunga hattrick katika mashindano hayo pale alipofunga magoli manne dhidi ya Cameroon katika ushindi wa magoli 7-0 kwenye mchezo wa hatua ya makundi.
Mshambuliaji huyo pia ndiye anaeshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa ligi ya ndani kwa ngazi ya vilabu na pia mfungaji bora wa michuano ya ukanda wa afrika mashariki na kati CACAAF, mafanikio aliyoyapata kabla ya hivi sasa kuwa ufungaji bora kwa bara la Afrika.

0 comments:

Post a Comment