BAO
pekee la kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod
Msuva usiku wa jana lilitosha kuipa Difaa Hassan El-Jadidi ushindi wa
1-0 dhidi ya wenyeji, FAR Rabat katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe
la Morocco Uwanja wa Manispaa ya Kenitra.Simon
Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga SC ya Dar es Salaam, alifunga bao
hilo pekee la ushindi dakika ya 23 katika siku ambayo alikuwa
anasherehekea kutmiza miaka 26 tangu azaliwe Oktoba 2, mwaka 1993.
Msuva
ambaye katika timu hiyo yupo pamoja na chipukizi mwingine Mtanzania,
Nickson Kibabage aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mtibwa Sugar jana
alicheza vizuri mno.
Simon Msuva akikimbia kushanglia na wachezaji wenzake baada ya kuifungia bao pekee Difaa Hassan El-Jadidi ikiilaza 1-0 FAR Rabat jana
Na baada ya mchezo huo, wachezaji wa Difaa Hassan El-Jadidi walianza kumuimba nyota hiyo wa Tanzania hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo.
Difaa Hassan El-Jadidi watateremka tena dimbani, Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan Jumapili kumenyana na Wydad Casablanca katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco kuanzia Saa 3:00 usiku.

0 comments:
Post a Comment