Wednesday, October 9, 2019



Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali  amefunguka kuwa bado hali yake sio nzuri lakini viongozi wa Yanga licha ya kwenda klabuni lakini bado hawajamsaidia kitu chochote.

Mzee Akilimali kwa siku za karibuni amekuwa akiugua na akiomba msaada wa matibabu yake kutokana na matatizo ambayo yanamkabili kiafya.

Mzee huyo alisema hali yake kwa sasa siyo nzuri kwani anashindwa kuona na sauti yake inakauka kutokana na  ugonjwa wa sukari unaomsumbua.

Akilimali alisema kuwa  amekuwa akijaribu kuomba misaada ya hapa na pale lakini hata viongozi wa Yanga wameshindwa kumsaidia licha ya kwenda pale klabuni hapo.

“Ukweli bado hali yangu siyo nzuri kadiri siku zinavyokwenda, nashindwa kuona  lakini nashangaa viongozi wa Yanga wanashindwa hata kunisaidia, nimekodi Bajaj kwenda pale baadhi yao wameniona lakini hamna kitu.

“Viongozi wanatakiwa kujua sisi kwenye soka toka zamani tulikuwa tunasaidiana na tunaheshimu wazee.”

0 comments:

Post a Comment