David
Moyes ameteuliwa kuwa meneja mpya wa West Ham na atarejea kwa mara ya
pili kwenye klabu hiyo. Mscotland huyo mwenye miaka 55 amesaini mkataba
wa miezi 18 na ataanza na mechi ya nyumbani ya siku ya mwaka mpya dhidi
ya Bournemouth.
Moyes anachukua mikoba ya Manuel Pellegrini,
aliyetimuliwa baada ya kushindwa mechi ya Jumamosi 2-1 nyumbani dhidi ya
Leicester wanaoonekana kubadilika sana.
Kocha
huyo wa zamani wa Everton na Manchester United, aliyechukua mikoba
kutoka kwa Slaven Bilic miaka miwili iliyopita, aliondoka mwishoni mwa
msimu, baada ya klabu hiyo kuamua kuelekea upande mwingine na meneja wa
zamani wa Manchester City Pellegrini.
Lakini
Mchile huyo aliyeiongoza Hammers na kuwa nafasi ya kumi msimu uliopita,
ametimuliwa kufuatia kushindwa mara nne mfululizo nyumbani juzi
Jumamosi. Stuart Pearce na Alan Irvine, waliokuwa wasaidizi wa Moyes
hapo nyuma, wanaweza kuwa tena wasaidizi wa kocha huyo.
0 comments:
Post a Comment