DITRAM Nchimbi, nyota mpya wa Yanga amesema kuwa atapambana kufikia malengo yake pamoja na timu kwenye timu yake mpya ya sasa.
Nchimbi amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea timu ya Polisi Tanzania alikokua kwa mkopo wa mwaka mmoja alikuwa ni mali ya Azam FC.
Nchimbi tayari ameanza mazoezi na timu yake mpya ya Yanga ambayo leo inashuka uwanja wa Taifa kumenyana na Biashara United ya Mara.
"Nipo na furaha ndani ya Yanga na kila mmoja anatambua kwamba kwa sasa nipo sehemu salama ambayo ina ushindani mkubwa na kila mmoja anaushirikiano na mwenzake kikubwa ni kupambana kufanya vema na mashabiki watupe sapoti," amesema.
Yanga ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 10 huku Biashara United ikiwa nafasi ya 15 na pointi zake 15 baada ya kucheza mechi 13.
0 comments:
Post a Comment